Kuanguka Kwa Soko la Bidhaa za Asili
Ni Wangapi wana picha za asili zinazoonyesha na kudhibitisha tamaduni zao? achilia mbali picha za ukutani ambazo mara nyingi hutumika kama mapambo ndani ya nyumba lakini pia nadharia ya kusikiliza nyimbo zinazoelezea mila, desturi za Afrika nazo kwa sasa zimetupwa miongoni mwa Waafrika wengi. Ni mali ambazo zinazidi kuanguka kisoko hasa katika soko la ndani. Imekaririka kuwa wanaopenda kununua bidhaa hizi ni watu wa nje wanaokuja kutembelea Africa.
Tafiti zilizofanywa na OPEN AFRICAN MAGAZINE zimeonesha kuwa, wanaofanya manunuzi ya mara kwa mara ya bidhaa za asili ni watu kutoka nje ya Afrika, magazine hii ilitembelea maeneo mbalimbali zinapopatikana bidhaa hizi za asili na kugundua asimilia kubwa ya wanunuzi wa bidhaa hizi, ikiwa ni wageni kutoka nje ya nchi hususan bara la Ulaya na hivyo kufanya bidhaa hizi kuwa na soko la watu kutoka nje ya Afrika na wazawa yaani (Wa-Afrika) kuwa na muitikio mdogo kununua bidhaa asili.
0 comments:
Post a Comment